Tottenham walifungua mlango katika nusu ya pili wakati Emmanuel Adebayor alipofunga bao lake la kwanza tangu mwezi wa Mei.
Westham walisawazisha kupitia kwa Matt Jarvis na
zikiwa zimesalia dakika tano mchezo huo kumalizika, Modibo Maiga
alifunga kwa kichwa kutokana na krosi ya Mohamed Diame.
Mechi hiyo ilianza tu kusisimua katika dakika ya
67 pale Adebayor, ambaye hadi wakati huo alikuwa amecheza kwa jumla ya
dakika 45 tu msimu mzima alipofunga bao. Lakini hatimaye Spurs walitoka
wakiwa wamepigwa na butwaa kutokana na kipigo cha pili mfululizo
nyumbani kwao wiki hii baada ya kuchapwa 5-0 na Liverpool, siku ya
Jumaapili na kusababisha kocha Andre-Villas Boas kupigwa kalamu.
Katika mchuano mwinginge klabu bingwa ya ligi ya
England Manchester United nao pia walipiga hatua ya kuingia nusu
fainali ya kombe hilo kwa kuicharaza Stoke City mabao 2-0 yaliyofungwa
na Ashley Young na Patrice Evra katika mchezo uliosimamishwa kwa muda
kutokana na mvua. Katika nusu fainali United wamewaepuka majirani na
watani wao wa jadi Manchester City,na watapambana na Sunderland
waliowatoa Chelsea siku ya Jumaanne.
No comments:
Post a Comment