![]() |
Juma Kaseja |
KIRAKA wa Yanga, Mnyarwanda Mbuyu Twite amesema yupo vizuri
kimazoezi tayari kwa lolote huku akitamba kuwa kikosi chao kimeongezewa
nguvu na kipa Juma Kaseja.
Mbuyu, ambaye kikosini hapo anachezeshwa kama beki
wa kulia, ingawa mara nyingine anacheza nafasi ya beki wa kati, kushoto
na kiungo hakuitwa kwenye kikosi cha Rwanda ‘Amavubi’ badala yake
alibaki Dar es Salaam kwa mapumziko.
Aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Kama unavyoona
tunafanya mazoezi, ndiyo tunajiandaa taratibu, binafsi najiona niko fiti
kwa sababu najua wajibu wangu, nimejiandaa na niko tayari kwa kazi.”
Akimzungumzia, Kaseja kuwepo kikosini mwao, Mbuyu
alisema: “Kaseja ni kipa mzuri na hata kwenye mazoezi unaona, uwepo wake
utaisaidia timu nzima na hasa safu yetu ya ulinzi kuhakikisha
haturuhusu bao.
No comments:
Post a Comment