![]() |
Kipa Abel Dhaira |
KIPA Abel Dhaira, ametamka kuwa anajua jambo kubwa lililofanya yeye kutemwa na Simba si kutokana na kushuka kiwango.
Akizungumza na Mwanaspoti, kipa huyo kutoka Uganda
alisema kuwa ametemwa Simba kwa madai kuwa alikuwa akiuza mechi mara
kwa mara na kufungwa kwake mabao matatu katika mechi dhidi ya Yanga
kulizidisha makali ya tuhuma hizo.
Dhaira ambaye kwa sasa yuko Kampala, Uganda
alisema: “ Kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuna
kiongozi ambaye alinituhumu kuwa mimi nauza mechi.
“Tena iliniuma sana kwani sikuona haja ya
kuihujumu timu yangu, nililenga kuisaidia Simba, hakuna kipa
asiyefungwa, mimi naweza kufanya makosa ya kibinadamu na lawama zikawa
za kuuza mechi, kwa kweli hata kama ningebaki tuhuma hizo zingeninyima
amani.
“Lakini naijua kazi yangu ndugu yangu, kwa mambo
wanayofanya Simba soka halitaenda kokote, itakuwa ni lawama kila
kukicha,’’ alisema
“Nakumbuka Kocha Kibadeni aliniambia nia ya
kumtumia kipa wa vijana Abou Hashimu kwenye mechi mbili za mzunguko wa
kwanza ili kumsaidia kipa huyo kupata uzoefu wa kucheza ligi na mimi
nililipokea hilo kwa moyo mmoja ili kumsaidia kijana huyo,” alisema
Dhaira.
Dhaira anakamilisha mipango ya kwenda nchini
Iceland Januari mwakani ambako huenda akajiunga kwa mara nyingine na
klabu yake ya zamani ya Vestmannaeyja ‘ÍBV’.
No comments:
Post a Comment