Dar es Salaam. Siku moja baada ya Yanga kutangaza kumsajili mshambuliaji Emmanuel Okwi, uongozi wa Simba umesema hauna ugomvi na mchezaji huyo licha ya kudai kufuatilia suala hilo Shirikisho la Soka Duniani (Fifa).
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are
‘Kinesi’ alisema wanachojua suala lao lipo Fifa na kama Yanga
wamemsajili hiyo ni shauri yao kwani uamuzi ya Fifa kuhusu malalamiko
yao bado haujatolewa.
“Etoel walimshtaki Okwi kwa Fifa, Okwi akawaeleza
wazi yeye hajalipwa mshahara wake miezi mitatu, pia miezi mitatu
hajacheza mechi hata moja ndiyo maana akaamua kuondoka, hivyo Fifa
walimruhusu kucheza Villa.
“Hatuna kesi na Okwi tuna kesi na Etoil du Sahel
watulipe fedha zetu, katibu (Evodius Mtawala) anafuatilia kuhakikisha
tunapata majibu ya uhakika leo hii (jana) ili tujue moja na
tutawajulisha kinachoendelea.” alisema Itang’are.
Jana Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto
alisema Okwi wamemsajili kwa muda wa miaka miwili na nusu na kuonyesha
ITC ya mchezaji huyo iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA)
baada ya kupata baraka za SC Villa.
No comments:
Post a Comment