Tuesday, 17 December 2013

KIAMA,ARSENAL MDOMONI MWA VIGOGO














Timu 16 zimeingia kwenye hatua ya mtoano, ambapo timu nane zilizoongoza makundi na nane nyingine zilizomaliza nafasi ya pili.
MARA kipyenga kinapulizwa, Arsenal dhidi ya Real Madrid kwenye mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hakuna ujanja, vinara hao wa Ligi Kuu England ikiwakwepa wababe hao wa Santiago Bernabeu, inaweza kuangukia kwenye midomo ya vigogo wengine hatari zaidi, PSG, Bayern Munich, Atletico Madrid au Barcelona.
Yote hayo yatafahamika leo, Jumatatu mjini Nyon, Uswisi wakati upangaji wa timu zitakazochuana kwenye hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakapofanyika.
Arsenal imeshika nafasi ya pili kwenye kundi lake, jambo linalowaweka kwenye hatari ya kukumbana na moja ya vigogo hivyo vilivyoongoza makundi yao.
Timu ambazo Arsenal inayonolewa na Mfaransa Arsene Wenger haitakumbana nazo kwenye hatua hiyo ya 16 bora ni ni Manchester United, Chelsea kwa kuwa ni za kutoka England na Borussia Dortmund kwa kuwa zilikuwa kwenye kundi moja.
Hii ni mara ya 14 kwa Arsenal kuvuka hatua ya makundi ya michuano hiyo, lakini kichapo cha Jumatano iliyopita dhidi ya SSC Napoli kimewaweka pabaya.
Baada ya michuano hiyo kufika hatua ya mtoano, akili za mashabiki wengi wa soka zinasubiri kufahamu nani atamkabili nani kwenye michuano hiyo baada ya droo yake ya makundi itakayofanyika mjini Nyon.
Timu zilizofuzu
Timu 16 zimeingia kwenye hatua ya mtoano, ambapo timu nane zilizoongoza makundi na nane nyingine zilizomaliza nafasi ya pili.
Wababe waliongoza makundi ni Manchester United, Real Madrid, Paris Saint-Germain, Bayern Munich, Chelsea, Borussia Dortmund, Atletico Madrid na Barcelona, wakati walioshika nafasi ya pili ni Bayer Leverkusen, Galatasaray, Olympiacos, Manchester City, Arsenal, Schalke 04, Zenit St Petersburg na AC Milan.
Ujerumani imeingiza timu nne sawa na England, hivyo kuna kila dalili timu hizo zikapangwa kumenyana hatua hiyo ya mtoano, huku Man City ikiwa na uhakika wa kuikwepa Bayern Munich kwenye mtoano kutokana na kupangwa kundi moja.
Timu nyingine ambazo Manuel Pellegrini na kikosi chake cha Man City inaweza kukumbana nazo ni Barcelona, Real Madrid, Atletico Madrid, PSG na Borussia Dortmund, sawa na Arsenal ambayo kwenye orodha ya timu hizo ni Dortmund tu ambazo hatamenyana nayo kwenye mtoano wa 16 bora.

No comments:

Post a Comment