
KOCHA wa Simba, Zdravko Logarusic kwa siku mbili mfululizo amekuwa akimpa mazoezi na mbinu mpya za ufungaji straika wake, Amissi Tambwe ili atishe kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe leo Jumamosi dhidi ya Yanga yenye kipa Juma Kaseja.
Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Zanzibar ilipo
kambi ya Simba, Tambwe alisema kocha amekuwa akimpa mbinu mpya za
ufungaji dhidi ya makipa wazoefu na wajanja kama Juma Kaseja wa Yanga.
“Naendelea vizuri na mazoezi na kocha ananipa
mazoezi mengine mapya ya kufunga mimi na washambuliaji wenzangu ili
tuweze kufanya vizuri katika mchezo na Yanga, kocha anataka tufunge
haraka na ametuambia tunaweza kufanya vizuri,” alisema Tambwe raia wa
Burundi.
Alipoulizwa na Mwanaspoti kama anamfahamu Kaseja,
Tambwe alijibu: “Namfahamu Kaseja kama kipa mzoefu na anayeweza kuzuia,
lakini mimi namwona wa kawaida kama walivyo makipa wengine.”
Tambwe, ambaye anaongoza kwa ufungaji katika Ligi
Kuu Bara, alisema: “Kwa nini nisifunge? Naomba nipate nafasi halafu
tucheze kwa kuelewana kikosini, mimi ni mshambuliaji ninayejiamini na
kazi yangu.”
No comments:
Post a Comment