Dar es Salaam. Pepo mbaya amezidi kuiandama
Simba baada ya wanachama wanaodhaniwa kuwa wa klabu hiyo wanaotoka
katika Matawi ya Mpira Pesa na Mpira Maendeleo kutwangana ngumi
hadharani.
Tukio hilo lilitokea jana asubuhi mtaa wa Msimbazi
yalipo makao makuu ya Klabu ya Simba ambapo uchunguzi wa Mwananchi
ulibaini chanzo ni tofauti za kimsimamo baina ya wanachama wa matawi
hayo mawili.
Mwananchi baada ya kufuatilia kwa kina lilibaini
kuwa wanachama wa Tawi la Mpira Pesa wanataka Mwenyekiti wa klabu hiyo,
Ismail Rage ajiuzulu kwanza wakati Mpira Maendeleo wanataka Kamati ya
Utendaji nzima ya iondoke madarakani.
Hata hivyo, purukushani hizo zilikoma baada ya polisi kufika eneo hilo na kuingilia kati kuyatawanya makundi hayo.
Kumekuwapo kwa mijadala miongoni mwa wanachama na
mashabiki wa Simba tangu mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Emmanuel
Okwi aliposaini mkataba wa miaka miwili na nusu kujiunga na Yanga
akitokea SC Villa ya Uganda ambayo alikuwa anaichezea kwa mkataba
maalumu wa miezi sita.
Wanachama na mashabiki wa Simba wamekuwa wakihoji
kulikoni Okwi asajiliwe na Yanga wakati klabu yao bado inaidai klabu ya
Etole Du Saleh Dola 300,000 za mauzo ya mchezaji huyo ambazo bado
hawajalipwa
No comments:
Post a Comment