Liverpool, England. Mshambuliaji Uruguay, Luis Suarez amekiri kuwa sasa amefanikiwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wa Liverpool baada ya kupitia katika kipindi kigumu mwaka huu.
Jumatatu, Suarez ameshinda tuzo ya mchezaji bora
wa mwaka 2013 ya William Hill Football Supporters’ inayotolewa na
Shirikisho la Mashabiki wa soka England.
Akipokea tuzo hiyo Suarez alisema “Liverpool najua
kwamba hadi Januari tutakuwa tukiwania kuendelea kubaki katika nne
bora, pamoja na kusaka ubingwa.”
Suarez alizikosa mechi sita za mwanzo wa msimu huu
kutokana na kufungiwa April kwa kitendo chake cha kumng’ata beki wa
Chelsea, Branislav Ivanovic.
Tangu amerejea uwanjani tayari ameshafunga mabao
17, pamoja na kuiongoza Liverpool kuisambaratisha Tottenham kwa mabao
5-0 Jumapili.
Kikosi cha Brendan Rodgers sasa kitaivaa Cardiff,
Manchester City na Chelsea kabla ya kumaliza mwaka huu na Suarez amekiri
kuwa mechi hizo ndizo zitakazoamua hatima ya Liverpool katika kusaka
ubingwa.
“Nafikiri ni rahisi sana kusema,” alisema nyota
huyo mwenye miaka 26, wakati alipoulizwa kuhusu nafasi ya Liverpool
katika Ligi Kuu.
“Kama tutaendelea kucheza kwa kiwango hiki katika
wiki mbili au tatu zijazo hakuna shaka kwamba tunaweza kutwaa ubingwa wa
ligi au kumaliza katika nne bora.
“Jambo la muhimu ni sisi kuendelea kuweka mawazo yetu katika mchezo unaokuja.
“Tunajua baada ya mechi ya Cardiff, tunamechi mbili ngumu zaidi.
Suarez pia aliwashukuru mashabiki wa Liverpool kwa
kuonyesha imani kwake baada ya kufungiwa, amekiri kuwa asingeweza
kuendelea kuwepo klabu hapo kama si wao kumuunga mkono.
Alisema: “Kurudi kucheza tena Anfield baada ya
kupita katika kipindi kigumu hiyo yote inatokana na mashabiki kuwa nyuma
yangu, ni kitu ambacho nilikuwa sikitegemei kabisa wakati niliporudi
uwanjani.
No comments:
Post a Comment