![]() |
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hanspoppe ameithibitishia |
Posted
Jumanne,Decemba10
2013
saa
9:17 AM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hanspoppe
ameithibitishia Mwanaspoti kuwa wamemtema rasmi kipa wao wa Uganda, Abel
Dhaira na nafasi yake itachukuliwa na Ivo Mapunda.
Wakati hali ikiwa hivyo benchi la Ufundi la Simba
limepigwa marufuku kuweka maji baridi katika mazoezi ya timu hiyo na
hakuna mchezaji anayeruhusiwa kunywa maji hayo ili kulinda afya zao.
Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic ndiye aliyeweka
sheria hiyo na Mwanaspoti limeshuhudia meneja Nico Nyagawa akisisitiza
kutowekwa maji hayo katika benchi lao.
Katika mazoezi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki
kwenye Uwanja wa Kinesi, jijini Dar es Salaam Kocha Msaidizi wa Simba,
Seleman Matola aliomba maji kwa Nyagawa naye akaambiwa yapo ya moto
ndipo Matola alipoulizia maji ya baridi.
“Kocha hataki maji ya baridi hapa, kama unataka
kunywa ya moto sema nikupe,” alisikika akisema Nyagawa akionekana
kutekeleza agizo la Logarusic.
Baada ya kuona hali hiyo, Matola alikataa maji hayo na kuagiza aletewe maji ya baridi.
Ilibidi nahodha Nassor Masoud ‘Chollo’ ambaye
hakufanya mazoezi kutokana na kuwa majeruhi, atoke nje ya uwanja huo
kwenda kumtafutia Matola maji ya baridi ambayo aliyapata dakika chache
baadaye.
Baadaye Logarusic aliliambia Mwanaspoti ni kweli
amewapiga marufuku wachezaji wake kutumia maji hayo kwani ni hatari kwa
afya zao wakiyatumia baada ya kuchemka mazoezini.
“Hali ya hewa ya hapa ni joto sana, haiwezekani
mchezaji ametoka kuchemka halafu moja kwa moja unampa maji ya baridi hii
ni hatari, nimewaambia sitaki kuyaona maji ya baridi hapa maana nataka
kulinda wachezaji wangu,” alisema Logarusic raia wa Croatia.
Timu kadhaa za Ligi Kuu Bara hata timu ya taifa
hutumia maji ya baridi zinapokuwa katika mazoezi yao huweka maji hayo
kwenye vyombo maalumu vya barafu.
Tangu kuwasili kwa kocha mpya wa Simba kumekuwa na
utaratibu mpya katika kikosi hicho kuanzia mazoezi pamoja na maisha ya
wachezaji kwa ujumla.
Kocha huyo amesema anataka kuwa na kikosi cha wachezaji wasiozidi 25, lakini pia amekuwa akitaka wachezaji wanaojituma tu.
No comments:
Post a Comment