Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa.
KATIBU Mkuu mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Selestine Mwesigwa, ameliambia Mwanaspoti
kuwa jambo atakaloanza
nalo akiingia ofisini ni kuziba mirija yote ya watu kujipatia fedha
isivyo halali kupitia shirikisho hilo. Muda mfupi baada ya Rais wa TFF , Jamal Malinzi,
kumtangaza Mwesigwa kushika wadhifa huo, Katibu huyo ameibuka akiliambia
Mwanaspoti kwa kusema: “Unajua hii ni nafasi nyeti katika chombo
kikubwa kama hiki ambacho kinaongoza soka la nchi nzima, mimi najipanga
kuzuia mianya yote ya ulaji fedha ndani ya TFF, bila kufanya hivi naweza
kushindwa katika kazi yangu.”
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 43 akiwa pia ni
mtaalamu wa mambo ya sheria na uhusiano wa kimataifa, alisema jambo
jingine atakalolifanyia kazi ni kuhakikisha weledi katika utendaji kazi
unazingatiwa huku kila mfanyakazi akiwajibika katika nafasi yake.
Alisema atashirikiana vyema na watendaji wengine
kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya muda mfupi na muda mrefu
inatekelezwa kwa wakati katika muda wote wa kazi yake.
Mtendaji mwingine mpya wa TFF aliyetangazwa na
Malinzi ni Evodius Mtawala ambaye anakuwa Mkurugenzi wa Vyama, Wanachama
na Masuala ya Kisheria.
No comments:
Post a Comment